Kuolewa na Mzungu ni ”mapenzi” au ni ”mali”? usikose WanawakeLive Mange Kimambi na Devota Johansen jnne hii

Published February 6, 2012 by wanawake1

Kesho tarehe 7 February katika kipindi cha Wanawake Live,tunao wake wa wazungu Mange Kimambi pamoja na Devota,wengi mtakuwa mnamkumbuka aliyekuwa mke wa marehemu Dandu,kweli wamefunguka mengi kuhusu Familia , Ndoa na watoto. Kwa undani zaidi kuna Mengi ambayo wamefungua ambayo hayajawahi kuongelewa popote,wamefunguka ndani ya wanawake Live.

Super Woman Joyce Kiria akifungua show ya Wanawake Live

hahahahahhaahahaha kicheko cha Joyce Kiria unajua nini kilichomfurahisha ndani ya kipindi kesho

Super Woman Joyce Kiria akiwakaribisha wageni wake Mange Kimambi na Devota.

Mama Lincon a.k.a Super woman akisisitiza jambo ndani ya kipindi cha Wanawake Live.

Devota Johansen akiongelea jambo ndani ya kipindi cha Wanawake live,Jua mengi kutoka kwake?Ana watoto watatu but she is Amazing n Fabolous she still looking hot and Sexy.

Muke ya Muzungu Mange Kimambi, kawaida ndani ya show ya Wanawake Live kucheka ni kitu cha kawaida,nae alifunguka vya kutosha.

Super Woman Joyce Kiria akimsikiliza kwa makini Devota Johansen.

Mange akichangia mada huku devota akimsikiliza kwa umakini kabisa.

Wamependeza vya kutosha, Dah amini usiamini wala hawakuambiana wavae nini ila ilitokea tu, wamekutana studio wote ndani ya BLACK,they look Hooooooooot.

Muda ulikuwa mdogo mno kiukweli Mange na Devota walikuwa na mengi mengi ya kuongelea , ila walifunguka mengi .

Msikose kabisa kuangalia Wanawake Live Show kesho saa tatu kamili ndani ya tinga number moja kwa vijana EATV.

Advertisements

MKURUGENZI WA BANK YA WANAWAKE TZ ATEMBELEA MAFUNZO YA WLIVE

Published January 31, 2012 by wanawake1

Haya mafunzo yamefanyika jmosi 28jan2012 kwenye ukumbi wa TCRA, ni mafunzo ya kumwendeleza mwanamke bila kujali itikadi wala kabila, hadhi, na kila aina ya tabaka….

Strong Woman Joyce Kiria akifungua mafunzo ya kumkomboa mwanamke kimapinduzi ktk ukumbi wa TCRA barabara ya Sam Nujoma …

Super Woman na Mkurugenzi wa Bank ya Wanawake Tz Mama Magreth Chacha akizungumza na wajasiriamali na kuwafundisha mbinu za kupata mikopo huku akiwaahidi kuwapa mikopo endapo watazingatia mafunzo wanayopata, pia alisisitiza kwamba UMASKINI wa mtu huletwa na mtu mwenyewe na kuwahimiza wjizatiti kuondoka kwenye umaskini kwa kuwa INAWEZEKANA..

kwa maneno mengine ni kwamba kama mtu hajakuwa tayari kuuaga umaskini basi hata umfundishaje hatang’oka ng’o.. hata um’bebe na winchi hatabebeka, kwa hiyo kabla hujaja kupata mafunzo kwanza jiulize umejiandaa kuachana na umaskini?? umaskini ni ugonjwa unaotibika lakini tiba ya kwanza inatoka kwako.

Mwalimu wa semina zetu Ringo Mowo akiendelea na ratiba ya kutoa mafunzo katika mkutano wa jmosi iliyopita. semina ilianza kwa kupata shuhuda kwa baadhi ya watu ambao tayari wameshachukua hatua za kuuacha umaskini

Safari hii watu walifurika sana, ukumbi haukutosha, tupo kwenye changamoto ya kupata eneo kubwa zaidi …

Arafa Arobaini ni mjasiriamali aliepiga hatua baada ya kufatilia kipindi cha Wanawakelive msimu wa kwanza, kwa sasa anazidi kuendelea mbele na hapo alimkabidhi Super Woman zawadi za nguo alizotengeneza mwenyewe, kofia , sketi, nguo za mtoto wa Joyce Kiria…

jmosi ya 04/02/2012 semina itafanyika Ustawi wa Jamii barabara ya sinza (BAMAGA) na jmosi ya 11/02/2012 kutakuwa na semina ya watu wote.. endelea kututembelea ili ujue itafanyika wapi….

SHUKRANI KWA TIMU YA MABADILIKO HAYA , RINGO MOWO, JOSEPHINE SLAA, SUZAN MREMA, MWANASHERIA WETU DADA GRECY….

MAFUNZO YA WANAWAKELIVE KUWAUNGANISHA WAJASIRIAMALI NA MABANK ILI KUPATA MIKOPO

Published January 27, 2012 by wanawake1

Mafuzo ya Wanawakelive tumeyaboresha kwa kuwaunganisha wajasiriamali na BANK mbali mbali ili waweze kupata mikopo ya kuendesha ama kuanzisha biashara ili kujiletea maendeleo zaidi….

Strong Woman Joyce Kiria akifungua semina

Ringo Mowo mwalimu na muwezeshaji kwenye semina

Dk Josephene Slaa balozi wa WanawakeLive….

Hiyo ndo timu ya kujitolea ya Wanawakelive  inayofanya semina za kuwaendeleza wanawake, Joyce Kiria, Ringo Mowo, Josephene Slaa na Bi Suzy…

Anafanya biashara mbalimbali kama kuuza mboga mboga, maandazi, chapati, viatu, vitenge n.k   kupitia semina ameshasajili kampuni ya ukandarasi na anatarajia kupata mkopo ili afanikishe ndoto yake ya kuwa Bilionea… INAWEZEKANA

Amesomesha watoto kwa biashara ya chapati hadi kufika chuo kikuu, kupitia semina amejua ni jinsi gani ya kujiendeleza zaidi 

Alikuwa anauza vitu kwa kuzunguka ”mmachinga” Baada ya kufanya nae kipindi cha Wanawakelive na kubadilishana uzoefu na wanawake waliofanikiwa ,leo amefikia hatua ya kukodi fremu na biashara yake inazidi kukua, na sasa semina zinaendelea kumpa mbinu zaidi za kupiga hatua mbele….

Wanawake wakishuhudia namna mafunzo haya yalivyokuwa chachu ya mafanikio na tayari wameshaona mabadiliko..

Tukifuatilia mafunzo yatakayobadilisha kabisa maisha yetu….

Bi Suzy ni  Mshauri yupo katika timu ya ukombozi wa mwanamke kwenye Wanawakelive, amebobea zaidi kwenye saikolojia, ni mwanamke anafundisha masomo ya kujiamini na kujitambua kuthubutu n.k….

Dk Josephine Slaa katikati ya Waathirika wa mafuriko ”wapangaji” wanaoishi nje ya shule ya B. Mkapa nao walipata fursa ya kujifunza zaidi jinsi ya kuanza maisha na kufanikiwa ,  majaribu yanakuja kutokana na sababu , yawezekana bila mafuriko wasingepata elimu wanayoipata ambayo itaenda kuwabadilisha kabisha na kuwa mabilionea wa siku zijazo….

 

28 jan 2012 tutaendesha semina nyingne kwenye jengo la TCRA , pamoja ba semina tumewaalika Bank ya Wanawake TWB na Stanbic Bank ili watoe mikopo kwa wahitimu wetu ambao wataonekana wameelewa na wataweza kufanya biashara na kurudisha mikopo…

Tumeshaongea nao na kwa upande wa bank ya Wanawake atakuja mkurugenzi Mama Magreth Chacha, na upande wa Stanbic atakuja Johari Kelvin ambapo yeye ni Business Banker..

Ni wakati wako wa kujiletea maendeleo kamwe usikubali kubaki nyuma..

WANAWAKELIVE NI MAPINDUZI YA MWANAMKE/ MAENDELEO YA MWANAMKE/ KWA KILA MWANAMKE…

TUNAWASHUKURU SANA TCRA KWA KUSAPOTI MABADILIKO HAYA KWA KUTOA UKUMBI WAO BURE KABISA

 

 

DAWA ZA KUBUSTI NGUVU ZA KIUME ZINAONGEZEKA! MH JERRY SLAA NA RINGO MOWO ON WANAWAKELIVE ;;WANAUMELIVE”

Published January 27, 2012 by wanawake1

Katika harakati za kumkomboa mwanamke kimapinduzi Wanawake Live ilifanya kipindi na Wanaume live, ili kujua mitazamo ya wanaume kuhusu harakati hizi.

Strong Women Joyce Kiria ndo host wa kipindi hiki….

Mh Jerry Slaa na Super Woman Joyce Kiria

Mjasiriamali Ringo Mowo kwenye Wanawake Live ya ”WANAUME LIVE”

Pamoja na mambo waliyozungumzia ni tatizo kubwa la kupungua kwa nguvu za kiume kwa baadhi ya wanaume, sababu za wanaume kuhofia wake zao wakipata maendeleo ndoa au mahusiano yao yatayumba…

Shukrani kwa maduka ya Amina Design K.koo na Quality Center Pugu Road kwa kumvalisha Super Women Joyce Kiria….

Hawa ni mabilionea wa siku za mbele

Published January 23, 2012 by wanawake1

WanawakeLive ikitoa mafunzo ya kujitambua na namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika maisha, kufundisha maana ya ”MAFANIKIO” ukiweza kitatua matatizo yanayokukabili ndiyo maana ya mafanikio, kwa hiyo hata kwa wahanga wa mafuriko wanaweza kutatua tatizo lao kwa kukubali hali na kujifunza namna ya kuanza maisha upya badala ya kuendelea kukaa nje na kuililia serikali…..

Wanawakelive ni tumaini jipya kwa wahanga wa mafuriko wanaoishi nje kwa sasa kwani pamoja na kuwapelekea samaki mara kwa mara, siku hii tulienda na nyavu za kuvua samaki na kuwafundisha namna ya kuvua samaki….

Wahanga walituahidi kuanza maisha upya na kupambana na hali halisi waliyonayo baada ya kuwapa somo la kujitambua na ujasiriamali. badala ya kutegemea misaada kila kukicha wanaweza kujifafutia wenyewe riski ili maisha yao yaendelee. Wanawake live tunaamini kwamba kila jambo lina sababu ilibidi hawa wapate tatizo ili tukawape mbinu za mafanikio ili miaka ijayo wawe mabilionea….

SERIKALI HII IMELAANIWA, MWANAMKE AZALIA BARABARANI CHINI YA MTI NJE YA SHULE YA MKAPA

Published January 23, 2012 by wanawake1

 

Mama BAHATI ni mmoja kati ya wahanga wa mafuriko  wanaosota nje ya shule ya Mkapa kutokana na SERIKALI kuwanyanyapaa na kuwaita wapangaji ilihali janga wamepata wote. Mama BAHATI alikuwa mjamzito na sasa amejifungua mtoto wa kiume, kwa ushujaa wa mama huyu pamoja na shurba anazozipitia za kulala nje na kuzalia nje bado amempa mtoto wake jina lenye matunaini, BAHATI… Hongera sana mama Bahati , wewe ni shujaa na umedhihirisha kwamba mwanamke ni MAMA anaetakiwa aheshimike bila kujali hali aliyonayo au hadhi aliyonayo..

WanawakeLive tulikuwa tumekamilika, hii ndo team yangu ya kutoa mafunzo mbalimbali yakiwepo ya ujasiriamali na jinsi ya kupata mikopo na kuitumia na kuwaunganisha na mabank, maswala ya sheria, stadi za maisha, kujitambua wewe ni nani na unapaswa ufanye nini kwa wakati gani, namna ya kukabiliana na changamoto bila kujali ni kubwa au ndogo, bila kujali mazingira uliyonayo n.k….

Ringo Mowo akitoa somo kwa waathirika wa mafuriko ambao wanaishi nje, namna wanavyotakiwa kuikabili changamoto waliyonayo na kuanza maisha upya. INAWEZEKANA

Bi Suzy ni mtaalam wa saikolojia, nae akitoa maneno ya kuwatia moyo na jinsi ya kuanza maisha upya 

Simon Rusigwa, nae aliwasisitiza wahanga kwamba MAFANIKIO YA MTU YANALETWA NA MTU MWENYEWE, wanapoendelea kukaa pale nje hawamkomoi yeyote zaidi ya kujikomoa wao wenyewe. ni wakati sasa wakubali kuanza upya, midhali wana afya, hawakufa wala kupata ulemavu basi inawezekana kabisa kuanza upya…..

walitoa baraka zao kwa watoto hawa, waje kuwa mabilionea wa kizazi kijacho

Baada ya kuwafundisha namna ya kuvua SAMAKI walifurahi sana na walibadilika mitazamo yao ya awali ambayo ilikuwa kuendelea kuisubiria serikali, na wakajizatiti wataanza maisha upya wakitumia elimu tuliyowapa. Shukrani kwa Team ya Wanawake live ambao wanajitolea kuleta mapinduzi kwenye Taifa hili….

 


 

 

WANAWAKE LIVE TUTAKUKUMBUKA DAIMA MAREHEMU REGIA MTEMA.

Published January 17, 2012 by wanawake1

Marehemu Mh. Regia Mtema, sisi wanawake Live tutakukumbuka daima, ulitusupport kwa hali na mali pale tulipokuhitaji,hakika Taifa limepoteza Mwanamke mpambanaji hususani Wanawake na watu wenye ulemavu. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi.Ameen

Super Woman Joyce Kiria akisisistiza jambo ndani ya wanawake live show 

From left Mboni Masimba a.k.a Kim K wa Bongo, Hilda Mallomo, Janeth Sinda and Super Woman mwenyewe Joyce Kiria ndani ya Wanawake Live.

Kim Kardashian wa Bongo, Akifunguka bila kificho ndani ya show.

Mjasiriamali ndani ya show.

Tabasamu muhimu mjasiriamali akijiachia kwa raha zake.kucheka kunaongeza siku za kuishi.

Super Duper Woman Joyce kiria akisisitiza jambo ndani ya show.

Warembo wakiwa wanasikiliza kwa umakini ndani ya wanawake live.

Jambo likieleweka pozi kama hizi ni kawaida kuja automatically.

Janeth sinda akisisitiza jambo huku Hilda akimsikiliza kwa umakini.

Vicheko ni kawaida ndani ya show ya Wanawake live,unataka kujua why they lough? dont miss out leo usiku.

Umakini ni muhimu pale maongezi yanapokolea so watch out leo usiku.

Usikose kutazama show leo saa tatu kamili usiku ndani ya EATV.