Archives

All posts for the month December, 2011

Yalianza masaa, siku, miezi now we just count some hours to finish da year

Published December 31, 2011 by wanawake1

Hello,

Ilikuwa saa ,masaa, siku, miezi now tayari tumebakiza masaa kadhaa kuufunga mwaka huu na kuanza mwaka mpya ,,kubwa ni kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu tupe uzima tupate kuuona mwaka 2012,,Namshukuru Mungu niko salama mimi pamoja na familia yangu na pia naamini wote huko mliko mpo salama,,ila kama yupo mgonjwa kwa hali yoyote ile namuombe Mungu amjalie afya njema.

Jamani jamii yote kwa ujumla tuendelee kubaki na amani na utulivu katika kuukaribisha mwaka mpya…

Endelea kutazama Wanawake Live nawaahidi mimi pamoja na timu yangu kuwaletea mambo mazuri yaliyo hot hot hot.          

Wanawake tuliofanikiwa tuwainue wanawake wa chini.

Published December 27, 2011 by wanawake1

Kutokana na Maombi ya watazamaji wengi haswa ambao walikosa semina iliyofanyika dar

Tumeona ni vyema kuwaalika studio watoa mada wa semina ile Bw.Ringo Mowo na Dr.Josephine Slaa

Mwanaharakati wa ukweli Joyce Kiria, huyu ni mwanaharakati kamilikwa kuamua kuwakomboa wanawake kwa vitendo

zaidi na imeonekaka fika hizi semina zitawasaidia wengi mno kubadilika na kupata maendeleo.

Dr.Josephine Slaa ni mwanamke ambaye naweza sema ni jasiri na mwenye kuthubutu, na amedhihirishaMafanikio ni safari 

yenye milima na mabonde,alianza kuuza mkaa na sasa anamiliki Precious Clinic.

Bwana Ringo Mowo ni mmojawapo ya wakinababa wa kuigwa ameongea maneno mazuri kumgusa mwanamke

Trust me unataka kufahamu ameongea nini kuhusu mwanamke? watch out EATV leo usiku.

Dada Domitila ni mwajiriwa na pia ni mfanyabiashara na yeye kafunguka vya kutosha ndani ya wanawake Live

Huyu dada amenifurahisha sana, na ameonyesha changamoto ya kweli na kwa wengine,kweli hizi mada zinasaidia

alikuwa mfanyabiashara,akakata tamaa kabisa wakati biashara haikwenda vizuri,ila baada ya kipindi hiki ameahidi

kurudi kwa nguvu zote katika biashara na amekiri kuwa ameongezewa ujasiri wa ajabu.

Bwana Ringo akisisitiza jambo huku Super Woman Joyce Kiria akisikiliza kwa makini.

Dr.Josephine Slaa Akisisitiza jambo.

Usikose kutazama Wanawake Live leo saa tatu kamili usiku EATV.

NB: Endelea kutembelea blog yetu tutazidi kuwaabarisha mambo mengi kubwa ni kuhusu semina ambazo

Zitaendelea baadhi ya Mikoa, japo lengo letu kubwa ni kufika Mikoa yote ya Tanzania,kwa kuwezesha hili

tunawaomba wadau kuchangiaSemina hizi kwa chochote ambacho utajaliwa, ukiweza kutoa pesa, kutudhamini kumbi

kwa ajili ya kufanyia semina hizi, kutudhamini usafiri kutoka Dar kuja katika mkoa wako, 

Shukrani: Shukurani za Dhati kwa Bi Lulu wa Morogoro kwa mchango wako wa Tsh 50,000 katika kufanikisha semina.

Hata wewe unaweza kuchangia kwa M-PESA kwa namba hii +255 753 787 126

 

 

HAPPY BIRTHDAY SUPER WOMAN JOYCE KIRIA

Published December 25, 2011 by wanawake1

Kila tarehe 26 December, Unakuwa unakumbuka siku yako maalum ya kuzaliwa.

Hii ni Special Day ikiwa inaenda sambamba na Boxing Day.

Wewe ni mmojawapo ya wanawake wapambanaji katika harakati za kumkomboa mwanamke.

Super Woman Joyce Kiria.

Wishing You So many Years ahead mamii ili uendeleze mapambano katika kumkomboa Mwanamke.

Happy B.Day mamii a.k.aMama Lincon a.k.a Mrs Henry Kilewo

Ukitoka Moshi keki inakusubiri huku.

Says ya’  Producer Wanawake Live Hellen Baja.

Kibaja Family,Hilda Mallomo na Wanawake Live Wapeleka misaada mchikichini

Published December 23, 2011 by wanawake1

Hizo ni nguo toka kwa Hilda Mallomo Kimara, Kibaja Family Kurasini na Super Woman Wanawake Live Joyce Kiria…

msaada zaidi unahitajika

            

Harakati za kukabidhisha mizigo ya nguo, shukrani kwa Kibaja Family Kurasini na Hilda Mallomo wa Kimara

Kidogokidogo hujaza kibaba, kama tukijitolea kwa kadri Mungu atakavyotuwezesha tutawasitiri Wanawake wengi sana

uwezo tunao tafadhali tujitoe kwa dhati ya Mioyo yetu ……Bado msaada zaidi unahitajika

 

WanawakeLive imekuwakilisha mafurikoni

Published December 23, 2011 by wanawake1

Supa Woman Joyce Kiria akiwakilia WanawakeLive kwa kila Mwanamke,

amepeleka  Salam za pole kwa wanawake waliopata janga la mafuriko.

Akitoa salamu za pole na kuwahasa wanawake wamshukuru Mungu kwa kila jambo wakati yeye pamoja na

wadau wakijitoa

kwa hali mali ktk wakati huu mgumu sana kwenye historia ya maisha yao…

Huyu ni mama wa watoto kumi akiwemo Mh Zitto Kabwe

Published December 21, 2011 by wanawake1

Ukiona vinaelea ujue vimeundwa. Huku ndo safari ya Wanawake Live ilikoanzia.

Tulipoanza wazo lilikuwa ni kuwaalika washiriki a.k.a Audience kama utakavyowaona hapo chini.

Wanawake Live ilianza rasmi kurekodiwa 2009 ,even if haikupata nafasi ya kwenda hewani. 

Wazo la kuwa na Audience bado lipo linafanyiwa kazi, je utapenda kushirikiiiiiiiii???????????? stay tuned hapahapa bloguni tutakupa taarifa….

Ilikuwa ni mwaka 2009, ndipo mchakato wa WANAWAKE LIVE ulianza rasmi kurekodiwa…

Mama Shida Salum ambae ndo M/Kiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu Tz alikuwa mgeni Maalum….

Tulijipanga kuwa na Audiance watazamaji kama unavyoona, changamoto ni studio! lengo bado lipo tunachoomba ni tupate studio kuuuubwa.

Shida Salum, Huyu ni mama wa watoto 10 akiwemo Mh Zitto Zuberi Kabwe…kilio chake ni miundo mbinu kwa Wanawake  wenye ulemave haswa wakati wa kujifungua…

Kylin, Irene, Nargis na Hawa wamefungukajeeee kwenye Wanawake Live Leo

Published December 20, 2011 by wanawake1

Super Woman Joyce Kiria akifanya vitu vyake kwenye show ya Wanawake Live

Aliyewahi kuwa Miss Tz na mrembo asiyezeeka Jacklin Ntuyabaliwe a.k.a Kylinn akijiachia kwenye bonge la show ya Wanawake Live….. Leo saa tatu usiku

Kutoka Bongo Real Mamaz a.k.a BRM Mamaa  Irene nae akiwakilisha vyema kabisa

Miss Tz no 3 enzi za Slivia Bahame, mamaa Nargis a.k.a Pam ndani ya Wanawake Live

Watu weweeeeeeeee, cheko lako tu mama Whiteley, umependezajeee, muite Hawa nae yupo kwenye Wanawake Live

Mazungumzo yamenoga sana hapo, usipitwe kuangalia Wanawake Live

Kylinn na Irene ndani ya Wanawake Live wakitupa dondoo za urembo(kuzaa si kuzeeka)

Nargis na Hawa wakitupatia tips za namna unavyoweza kuwa mama na ukarudi kuwa msichana mrembo.( kujisahau na kuacha rafu , uchafu, haihusu kabisa)

Mwongozaji wa kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiria akiwatupia maswali yake!!

Wanawake Live siyo ya kukosa, ni kila j4 saa tatu usiku EATV…

Badili Mtazamo Kwa kuchangia MAENDELEO kama tunavyochangia SHEREHE

Published December 19, 2011 by wanawake1

Hao ni Mabalozi wa WANAWAKE LIVE ambao wamewezesha Semina ya kuwapa wanawake mbinu lukuki za kukabiliana na maisha na kubadili mitazamo yao kabisa ili kujenga taifa lenye maendeleo.

Mafunzo hayo tungependa sana kuyafanya nchi nzima. tunaomba sapoti yako  ya hali na mali kwa kuchangia gharama kidogo za nauli kwa timu ya waandaaji kwa kutuma kwenye Mpesa +255 753 787 126 na CRDB 0150258750600

Baada ya kufanya Dar sasa tunajiandaa kwenda Arusha halafu baadae Mwanza, Tunawashukuru sana ARUSHA BUDGET SAFARIS kwa kutupatia vyumba bure ktk kuchangia maendeleo ya mwanamke tutakapokuwa Arusha.

Kwa upande wa Mwanza tunamshukuru Mkurugenzi wa LAKAIRO HOTEL kwa mchango wao wa vyumba tutakapokuwa Mwanza kwa ajili ya Semina hizo…

Hao wote ni MABALOZI wa WanawakeLive, WEWE JE????????

WATU 18 WALIOCHANGIA MAENDELEO YA MWANAMKE KTK KUFANIKISHA SEMINA DAR, 1 NI MWANAMKE, WENGINE NI WANAUME!!!

Published December 18, 2011 by wanawake1

Shukrani za pekee kwa uongozi wa TCRA kwa kukubali kuwa sehemu ya ukombozi wa mwanamke, kwa kukubali kutudhamini ukumbi wao mzuri na wa thamani kubwa sana, uliyowafanya wawe na furaha muda wote wa mafundisho. kwa kweli kinamama wanawashukuru sana walilia machozi pale tulipowapa ujumbe wa sapoti kubwa kutoka kwenu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA. Pia wanashukuru wafanya kazi mmoja mmoja kwa jinsi walivyoweza kujitoa kwa hali na mali, Mungu arudishe mara dufu pale mlipotoa…walichoahidi ni kufanya yale waliyofundishwa ili wawe chachu ya mabadiliko kwenye jamii, ambapo lengo letu ni kutokomeza UJINGA, UMASKINI, NA MARADHI kwa kasi inayolingana na hali yalisi ya Teknohama……

1. William Laiser – TCRA                             50,000/=

2. Wilfred Maro – TCRA                              50,000/=

3. Fransis Msungu –  TCRA                         50,000/=

4. Alinamuswe Kabungo – TCRA                 100,000/=

5. B.A. Haule – TCRA                                 30,000/=

Pia shukrani za dhati tena ni kwa MABALOZI wa wanawake kutoka UCC ambao wapo jengo la TCRA, kwa kuambua kuwa mstari wa mbele katika kumletea mwanamke maendeleo kwa njia ya kumpatia mafunzo yatakayomsaidia kwenye shughuli zake. Asanteni sana MBARIKIWE SANAAAAAA

6. Frank Tilugulkwa -mwajiriwa UCC                 10,000/=

7. Samueli Masasi – mwajiriwa UCC                 10,OOO/=

8. Emmanuel Natalis-  UCC                              2000/=

9. Alinani William – UCC                                   5000/=

10. Bernard Patrice – UCC                                 25,000/=

11. Moses Kehengu – UCC                              8000/=

shukrani nyingine ni kwa Viongozi wa ngazi y kitaifa, Mh Waziri Benard Membe na J.J. Mnyika, kwa kukubali kuwa Mabalozi wa WANAWAKE nchini kwa kuchangia au kuwezesha Semina kufanyika…..

12Benard K. Membe-  Waziri wa mambo ya Nje- 200,000/=

13. John J. Mnyika- Mbunge-                             100,000/=

Kwa namna ya kipekee WANAWAKE LIVE inampa BIG UP Dk Josephine Slaa kwa kukubali kuwa zaidi ya Balozi wa Wanawake, baada ya kuungana na wanawakelive kwenye mapambano ya kumkomboa mwanamke wa Tanzania bila kujali itikadi, dini, hata kabila, wala hadhi ya mtu… Tumeamua kuwa OMBAOMBA kwa ajili ya WANAWAKE WA TANZANIA…

14. Josephine M. Slaa- Mfanya biashara/ Clinic-  100,000/=

Ella, Maro,Komu, Munishi Kinamama wanawaombea sana popote mlipo, kufurahi kwao ni baraka kwenu, tuendelee kuwa pamoja kwenye mapinduzi haya ya kumkomboa mwanamke kimapinduzi… tumeanza na kumpatia maarifa ya kukabiliana na changamoto za uchumi, changamoto za mikopo, siri ya biashara, namna ya kudhibiti pesa, sheria ya biashara, namna ya kufanya masoko, n.k

15. Ella Ngoti-                                                   50,000/=

 16. A. I. Maro – Mr                                       30,000/=

17. Anthony Komu- Sirito Investiment        100,000/=

18. Deogratias Munishi – Bavicha –               20,000/=

     JUMLA                    1,003,000/=       

Unga mkono mapinduzi ya kumkomboa mwanamke kwa kuchangia kufanikisha SEMINA hizi ili ziweze kuwafikia mama, dada, wifi, semeji, bibi, zetu woooote waliopo vijijini….(Bi Suzi ni mwanamke aliyejitambua na kujiamini, leo hii amefanikiwa sana, anamiliki nyumba tatu na gari hapa mjini, Safari ya mafanikio yake ilianzia kwenye mama ntilie…huyo alievaa blauzi nyeusi na amefunga mkwiju kiunoni, HAPO AKIFUNDISHA NAMNA YA KUJIAMINI NA UNAAMBIWA KUJIAMINI KUNAANZIA JINSI UNAVYOTEMBE, UNAVYOONGEA, ULIVYOVAA n.k) Asante Bi Suzi kwa kukubali kuwa Balozi wa WANAWAKE……

MTAALUM ANAKWAMBIA KUISHI NI KUCHAGUA, KUWA MASKINI AU TAJIRI.. WEWE NDO UTAAMUA!!! KAMA WEWE NI TAJIRI SABABU NI WEWE, NA KAMA WEWE NI MASKINI SABABU NI WEWE…. KAZI KWAKO

UNAAMBIWA ELIMU YA DARASANI BILA KUJALI UMEVUKA VIDATO KIASI GANI, INACHANGIA 1% TU KATIKA MAFANIKIO YA MWANADAMU! 99% NI JUHUDI ZAKO ZA KUTAFUTA TAARIFA NA KUPENDA KUJIFUNZA KAMA UNAVYOPENDA KULA CHAKULA. PENDA SANA KULISHA UBONGO WAKO….(matajiri wengi duniani hawana elimu ya darasani, elimu yao ni ya kujifunza ktk maisha, WanawakeLive Joyce Kiria ndiko anakoelekea, alianza kufanya kazi za nyumbani housegal na sasa ni mtangazaji mkubwa Tanzania anairusha vipindi Afrika Mashariki na Afrika nzima kupitia DSTV) USIBAKI NYUMA…..

WANAWAKE WENGI TUNAPOTEZA MUDA MWIGI KUUGUZA MARADHI YANAYOTOKANA NA MAZINGIRA MACHAFU, HIYO NAYO NI SABABU NYINGINE YA WANAWAKE KUWA MASKINI. NI LAZIMA TUANZE KUJIJENGEA UTARATIBU WA KUSAFISHA MAZINGIRA YETU ILI TUEPUKANE NA MARADHI YASIYO YA LAZIMA….

UNGA MKONO KWA KUCHANGIA TSH 50, AU TSH 100, CHOCHOTE UTAKACHOGUSWA ILI HARAKATI HIZI ZISIRUDI NYUMA – MPESA +255 753 787 126- CRDB 0150258750600

Wafahamu Mabalozi wa kwanza kufanya mapinduzi ambayo hayajawahi kutokea

Published December 17, 2011 by wanawake1

Wanawake Live ikishirikiana na Mabalozi wa Wanawake Tz, Josephine Slaa na Ringo Mowo, iliandaa SEMINA ya kutokomeza UJINGA, UMASKINI NA MARADHI kwenye jamii yetu kupitia MWANAMKE.

Wanawake kadhaa tulipata fursa ya kuelimishwa na kufundishwa mbinu za kufanikiwa katika maisha, tulifundishwa namna ya kujua kipaji chako na kukifanyia kazi, tulifundishwa namna ya kupanga malengo na kuyatimiza, namna ya kupata mikopo na kudhibiti pesa, tulifundishwa sheria za biashara, pamoja na mbinu za kuuza biashara yako……

semina ilifanyika gorofa ya tatu jengo la TCRA, ambapo ilianza saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni….

Wanawake walianza kwa kujitambulisha wao ni nani na wanafanya nini, wamekwama wapi, wanaitaji nini, wanafahamu ndoto zao, wana malengo gani, n.k

Ukafika muda wa kumkaribisha Mwalimu/ Muwezeshaji wa semina yetu ili kile kilichokuwa kinakwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingi TUKIVUMBUE. Tukaanza kufatilia nukta kwa nukta, kituo kwa kituo huku tukiandika point tusijekusahau, maana lengo letu ni kuwa MABILIONEA wa siku zijazo…..

Wanawake tuna uwezo mkubwa sana wa kuwa mabilionea, tatizo siyo pesa wala mtaji, tunaitaji sana mafunzo ya ubunifu ktk shughuli zetu na namna ya kutafuta masoko, soko lako linataka nini…..mazagazaga ni meeeengi sana waliohudhuria semina walipata tumaini jipya….

Huu ulikuwa ni muda wa kunyoosha viungo na kuchangamka baada ya kukaa mda mrefu tukipata somo, zoezi hili liliendeshwa na Balozi wetu Josephine Slaa. mama yuko fiti huyo….

Ukafika muda wa kupata chakula huku wanawake wakitupia maswali ya hapa na pale kulingana na kile kilichofundishwa…… Endelea kutembelea blog yetu bado kuna picha nyingi tutaziweka na Tutakutaarifu Mabalozi wengine waliowezesha Semina hii  ya kuleta mapinduzi makubwa kupitia Wanawake Live wakiwepo Waziri na Wabunge..

Sisi ni ma Balozi wa Wanawake, je, WEWE ni Balozi wa Wanawake? uko tayari kuchangia MAENDELEO ya jamii yetu kwa kuwapa Wanawake Mafunzo kupitia Semina hizi???

Changia ulichonacho hata kama ni tsh 100/= ni kubwa sana kwetu na itafanya mapinduzi makubwa sana kwenye jamii yetu. kumbuka semina hizi zinaitaji Mwalimu (mtaalamu), ukumbi (sehemu ya kufanyia ) nauli kuwafata wanawake mikoani, hotel za kufikia, nyenzo za semina (pens,note book) n.k

Tunakukaribisha kwenye mapinduzi haya kwa kuchangia kupitia MPESA +255753787126 NA CRDB 0150258750600… UKIMKOMBOA MWANAMKE UMEKOMBOA FAMILIA, JAMII, NA TAIFA….

Wiki ijayo ni Arusha na Mwanza, KARIBU SANA….

Mjue Boyfriend wa Hadija Mwanamboka and did you know she has ten kids?

Published December 13, 2011 by wanawake1

Wanawake live kama kawaida leo ipo tena hewani, Mwanamapinduzi Joyce Kiria anaendeleza libeneke upande huo.

Mwanamapinduzi Super Woman Joyce Kiria.

 Mada kuu katika show ni transparent life kwa wapenzi. Pata kusikia mengi yaliyoongelewa kuhusu hilo. 

Mambo mengi yameongelewa katika kipindi mengi mno, likiwepo kuhusu boyfriend wa Hadija Mwanamboka.

Hadija Mwanamboka ndani ya Wanawake Live

Wakili Maria Mang’enya akiwakilisha ndani ya Wanawake Live

Mjasiriamali wa ukweli Eva Mushi nae akiwakilisha ndani ya Wanawake Live.

Mjasiriamali  Mzungu Bi Hellen, huyu mama kaongea mengi ambayo kweli wengi wenza tunafanyiana, usikose kutazama Wanawake Live umsikie mwenyewe.

Kipindi cha Wanawake Live kilinoga haswa na katika kuonyesha hilo vicheko vya hapa na pale havikukosekana.

Super Woman Joyce Kiria Akisisitiza jambo wakati wa show, kwa undani zaidi leo usikose kutazama Wanawake Live show saa tatu kamili usiku eatv.

 

kilewo: Bilioni 64 zimetumika kusherekea sherehe ya kuwanyonya watanzania.

Published December 12, 2011 by wanawake1

Sioni uhalali wa kutumia sh 64 billion za kitanzania kwaajili ya kusherekea Miaka 50 ya uhuru, Huku tukiwa tunamatatizo chungu nzima yanayo likabili Taifa letu. Nilidhani fedha hizo zingepelekwa kwenye miradi mbalimbali zikiendana sambamba na maadhimisho hayo ya miaka 50 ya uhuru.

Ingekuwa ni kilelezo tosha kusherekea miaka 50 ya uhuru huku hospitali zetu zikiwa zina dawa zakutosha, Akina mama kuwa na usafiri mathubuti wakati wa kukimbizwa kwenye hospitali, Tungetumia kuondoa kero ya  kuwalipa babu zetu mafao yao ya miaka nenda rudi, walimu wetu wangepatiwa malimbikizo ya mishahara yao ili washerekee sherehe hizo wakiwa kwenye mtazamo mpya wa maisha ya furaha badala ya kuwekea serikali yao chuki kutokana na kukosa jasho lao la halali.

Mwanamapinduzi Joyce kiria katika semina ya Wazazi na Watoto

Published December 12, 2011 by wanawake1

Kutoka kushoto ni Wanawake live, mama Aneth na Mama Morine

Tarehe 11 Dec  siku ya Jumapili kipindi cha Wanawake Live kiliandaa semina ya watoto na wazazi na mada ilikuwa ni mahusiano/mawasiliano kati ya mzazi na mtoto, katika kufanikisha hilo Mwanamapinduzi Super Woman Joyce Kiria alihakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Walialikwa wataalamu ambao walikuwa mahususi kwa ajili ya kuwapa somo wazazi pamoja na watoto ambao walihudhuria semina hiyo.Wataalam waliofika ni Aunty Sadaka, Bi Suzy na Ka Paul Hela.

Kupitia semina hii vilijulikana vitu vingi ambavyo vimejificha kutoka kwa watoto kwenda kwa wazazi,  na kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto. Yaliongelewa mambo mengi ambayo naamini toka siku ile yamebadilisha muelekeo mkubwa wa familia nyingi ambazo zilipata nafasi ya kuhudhuria semina.

Msimu Mpya wa Wanawake Live umedhamiria kwa dhati kuisadia jamii kwa karibu zaid,tayari Wanawake live imeanza kubadili muelekeo wa familia zetu huku mitaani katika swala zima la mawasiliano kati ya mzazi na mtoto.

Wanawake Live, Mama na Mwana.

Katika kukumbushana tu hapo ni mwanzo wanawake Live itazidi kuwaletea semina mbalimbali, kwa taarifa zaidi ni humuhumu,endelea kupitia humu.

Siri ya Kufanikiwa katika ujasiriamali

Published December 10, 2011 by wanawake1

Moja ya mikakati ya msimu wa pili wa show ya  Wanawake Live ni kumkomboa mwanamke kimapinduzi,hivyo basi wanawake live inakuletea semina mbalimbali zitakazokuwezesha wewe kupiga hatua kutoka hapo ulipo na kukusogeza katika mafanikio zaidi…Semina hizi zitaanza mapema mwezi huu kwa taarifa zaidi zitapatikana humu humu pamoja na katika kipindi cha wanawake live kinachokwenda hewani kila siku ya Jumanne saa tatu usiku eatv, marudio Jumatano saa nane kamili mchana na Jumapili saa nane na nusu mchana na African Magic Swahili channel DSTV.

Kwa yoyote atakayependa kushiriki semina hizi  Na kwa maelezo zaidi awasiliane na sisi kupitia

LOCAL MEDIA GROUP, WANAWAKE LIVE SHOW

JOYCE KIRIA 0783 137777

HELLEN BAJA 0682 717 434

Winnie Kalinga mwanamke shujaa alieingia kwenye TAKWIMU za vifo vya wajawazito na watoto

Published December 7, 2011 by wanawake1

Marehemu Winnie Kalinga ni miongoni mwa Wanawake mashujaa wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua kila baada ya saa moja….alifariki wakati wa kujifungua! inasikitisha sana  miaka 50 ya uhuru wa Taifa la Tz vifo vya kinamama wajawazito na watoto ni vya kutisha….RIP lv Winnie

Wanawake Live tunaomba viongozi wawajibike na kufanya majukumu yao ili kutokomeza janga hili kubwa kuliko tunavyodhani….

Wanakikundi wenzake na marehemu Winnie Kalinga, kushoto Mammy Hawa na Arafa ……..

BRM ya mtandao wa FB kwenye mazishi ya member mwenzao ambae kwa sasa ni marehemu Winnie…. RIP mamy

Mamaz wakiwakilisha….

Mamaz walokuja kumsindikiza rafiki kipenzi Winnie…..

Marafiki wa mume wa Winnie akiwepo Mafuru,  ndo waliandaa taratibu zote za maziko…