Hiki Ndicho Kishindo Cha Wanawake Live Msimu Mpya

Published December 2, 2011 by wanawake1

Huu ndo ujio wa msimu wa pili wa Wanawake Live, kauli mbiu ikiwa ni (WL ni kwa kila mwanamke) huyu ni mwanamke ambae ni corporate anaelekea kwenye meeting.. anakikao cha kiofisi, tunamuwakilisha vyema kwenye msimu wa pili wa Wlive….

Huyu ni dada wa club mwanzo mwisho, kila week end ni lazma akajirushe.. Wanawake Live kwa kila mwanamke, msimu wa pili ni balaaaaaaa

Huyu ni mwanaharakati wa haki za binadamu hasa za wanawake (Feminist) hatujakuacha popote ulipo, Wanawake Live kwa kila mwanamke, ni moto wa kuotea mbali usipitweeeee……

Huyu sasa ni hatari tupu, dada la twn, hapo mwenyewe hagusiki wala hakamatiki unaambiwa, she is hot hot hot, sexy, yaaani mwaaaa… tunamuwakilisha sana ndani ya Wanawake Live msimu mpya…usikoseeeeee

Mwanasiasa nae hatujamwacha nyuma, tunamuwakilisha vizuri tuu ndani ya WLive, usisahau safari hii ni kwa kila mwanamke jamanie…..

Umempata huyu??? Arusha wanamwita mjafanja wa town, yaani huyu ni wale madada wenye keshi yao (noti) akienda popote anajiamini na anauwezo wa kujihudumia kinywaji, msosi, malazi, ole wako ujichanganye eti wampa ofa ya bia, utaumbukaje???? atakutandika na kreti 5!!! hahahahahaaaaaa usipwitwe weeee

Huyu ni wale wadada wasiyopenda makorokoroz, hapo no nywele bandia (wigi) no bangiliz,  wenyewe wanajiita classic, anajipenda, anapendeza, hot n sexy kama kawa, tunamuwakilisha ndani ya msimu mpya wa WLive, usihadithiwe mwayegooo

OMG Fashenista umemuona? huyu hapitwi na wakati kabisa, tupo nae kwenye msimu wa WL….. usikubali abadani asilani kuhadithiwa, Kaa tayari mwenyewe kwenye luninga yako EATV…. watu weweeeeeee

Mamaa ya china, hong kong, Thailand, Dubai n.k, Mjasiriamali wa haja nakwambia hapo dili za biashara zimekubali, huyu nae tunae kwenye msimu wa pili wa WL kwa kila mwanamke….kauli mbiu unaipata lkn?????

Shost ndo kwanza katoka zake chuo (kamaliza chuo) anasaka kibarua a.k.a ajira, apoint ment haziishi jamani, sasa itakuwaje???? mwaya tupo pamoja kwenye WL

Jamani wanamichezo na wapenda gym woooote hatujawaacha kabisa, tupo nao bega kwa bega mpaka kieleweke…..WL this time ni kwa kila mwanamke…..yaani hakuna kudoz… 

 

Mwanamke urembo na sku hizi wanazidi kuwa wazuri jamani, asikudanganye mtu kuhusu kutupia na kupendeza, kumbuka mwanamke ni urembo bibi wee, wote ni kwenye WL Msimu mpya ndani ya EATV…….

Unarushiwa kiss hiyo ndugu yangu, amependeza na anajiamini,  swaga muhimu sana kwa madada duu, wala hataki shobo! hata wewe usijiache hovyohovyo usije ukajuuuuta, hahahahaaa usikose basi msimu mpya wa WL tuelezane ukweli………

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: