Mwanamapinduzi Joyce kiria katika semina ya Wazazi na Watoto

Published December 12, 2011 by wanawake1

Kutoka kushoto ni Wanawake live, mama Aneth na Mama Morine

Tarehe 11 Dec  siku ya Jumapili kipindi cha Wanawake Live kiliandaa semina ya watoto na wazazi na mada ilikuwa ni mahusiano/mawasiliano kati ya mzazi na mtoto, katika kufanikisha hilo Mwanamapinduzi Super Woman Joyce Kiria alihakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Walialikwa wataalamu ambao walikuwa mahususi kwa ajili ya kuwapa somo wazazi pamoja na watoto ambao walihudhuria semina hiyo.Wataalam waliofika ni Aunty Sadaka, Bi Suzy na Ka Paul Hela.

Kupitia semina hii vilijulikana vitu vingi ambavyo vimejificha kutoka kwa watoto kwenda kwa wazazi,  na kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto. Yaliongelewa mambo mengi ambayo naamini toka siku ile yamebadilisha muelekeo mkubwa wa familia nyingi ambazo zilipata nafasi ya kuhudhuria semina.

Msimu Mpya wa Wanawake Live umedhamiria kwa dhati kuisadia jamii kwa karibu zaid,tayari Wanawake live imeanza kubadili muelekeo wa familia zetu huku mitaani katika swala zima la mawasiliano kati ya mzazi na mtoto.

Wanawake Live, Mama na Mwana.

Katika kukumbushana tu hapo ni mwanzo wanawake Live itazidi kuwaletea semina mbalimbali, kwa taarifa zaidi ni humuhumu,endelea kupitia humu.

Advertisements

3 comments on “Mwanamapinduzi Joyce kiria katika semina ya Wazazi na Watoto

 • ongera sana dada joyce,nafurahishwa na kazi uifanyayo.mie ni mfatiliaji sana wa vipindi vyako toka bongo movie mpk wanawake live.nimeguswa sana na tukio la semina ya wazazi na watoto.nimeumia sijaweza kuwa part ya ilo tukio.mimi nimesoma sheria lkn ndani ya moyo wangu napenda kujiusisha na jamii.jamii haijui jinsi ambavyo watoto wanapitia wakati mgumu sana ktk ukuwaji wao mana wamekosa support ya wazazi.wazazi wa siku izi wako busy hawajui jinsi gani watoto tunavyowaitaji.nina mengi ktk ili jambo ila ntaishia apa pls naomba mfanye mara kwa mara semina iyo nami naomba niwe part ya semina iyo niko tayari kujitolea.tunaitaji kujenga jamii yetu na tuwe na watoto wenye msimamo,wanajitambua na waoweza kutubutu mana wanajiamini.lakini hayo yote yanaanzia nyumbani.ki ukweli malezi yanachangia sana kuwa na vijana tulionao sasa wazazi wetu wanatakiwa kujuzwa ilo.sofi

 • sophia na joyce,
  mi nataka niwakubushe kidogo 2. . . . .mana hao wazazi au wanawake wanapo kuja kwenye show ya wanawake live huwa wanasema 2 , wanaonesha huruma zao na watasema mengi ili wapate kusikika na sifa kwa jami wanaotazama show hiyo. . . .lakini vitendo hamna . . . . .
  Mi nasema na ninawambia hao wanaokuja kwenye show yako joyce… . . . . . . hebu acheni sifa zisizo na vitendo.
  Mutanisameh nikikosea plz.

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: