Wafahamu Mabalozi wa kwanza kufanya mapinduzi ambayo hayajawahi kutokea

Published December 17, 2011 by wanawake1

Wanawake Live ikishirikiana na Mabalozi wa Wanawake Tz, Josephine Slaa na Ringo Mowo, iliandaa SEMINA ya kutokomeza UJINGA, UMASKINI NA MARADHI kwenye jamii yetu kupitia MWANAMKE.

Wanawake kadhaa tulipata fursa ya kuelimishwa na kufundishwa mbinu za kufanikiwa katika maisha, tulifundishwa namna ya kujua kipaji chako na kukifanyia kazi, tulifundishwa namna ya kupanga malengo na kuyatimiza, namna ya kupata mikopo na kudhibiti pesa, tulifundishwa sheria za biashara, pamoja na mbinu za kuuza biashara yako……

semina ilifanyika gorofa ya tatu jengo la TCRA, ambapo ilianza saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni….

Wanawake walianza kwa kujitambulisha wao ni nani na wanafanya nini, wamekwama wapi, wanaitaji nini, wanafahamu ndoto zao, wana malengo gani, n.k

Ukafika muda wa kumkaribisha Mwalimu/ Muwezeshaji wa semina yetu ili kile kilichokuwa kinakwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingi TUKIVUMBUE. Tukaanza kufatilia nukta kwa nukta, kituo kwa kituo huku tukiandika point tusijekusahau, maana lengo letu ni kuwa MABILIONEA wa siku zijazo…..

Wanawake tuna uwezo mkubwa sana wa kuwa mabilionea, tatizo siyo pesa wala mtaji, tunaitaji sana mafunzo ya ubunifu ktk shughuli zetu na namna ya kutafuta masoko, soko lako linataka nini…..mazagazaga ni meeeengi sana waliohudhuria semina walipata tumaini jipya….

Huu ulikuwa ni muda wa kunyoosha viungo na kuchangamka baada ya kukaa mda mrefu tukipata somo, zoezi hili liliendeshwa na Balozi wetu Josephine Slaa. mama yuko fiti huyo….

Ukafika muda wa kupata chakula huku wanawake wakitupia maswali ya hapa na pale kulingana na kile kilichofundishwa…… Endelea kutembelea blog yetu bado kuna picha nyingi tutaziweka na Tutakutaarifu Mabalozi wengine waliowezesha Semina hii  ya kuleta mapinduzi makubwa kupitia Wanawake Live wakiwepo Waziri na Wabunge..

Sisi ni ma Balozi wa Wanawake, je, WEWE ni Balozi wa Wanawake? uko tayari kuchangia MAENDELEO ya jamii yetu kwa kuwapa Wanawake Mafunzo kupitia Semina hizi???

Changia ulichonacho hata kama ni tsh 100/= ni kubwa sana kwetu na itafanya mapinduzi makubwa sana kwenye jamii yetu. kumbuka semina hizi zinaitaji Mwalimu (mtaalamu), ukumbi (sehemu ya kufanyia ) nauli kuwafata wanawake mikoani, hotel za kufikia, nyenzo za semina (pens,note book) n.k

Tunakukaribisha kwenye mapinduzi haya kwa kuchangia kupitia MPESA +255753787126 NA CRDB 0150258750600… UKIMKOMBOA MWANAMKE UMEKOMBOA FAMILIA, JAMII, NA TAIFA….

Wiki ijayo ni Arusha na Mwanza, KARIBU SANA….

Advertisements

One comment on “Wafahamu Mabalozi wa kwanza kufanya mapinduzi ambayo hayajawahi kutokea

 • good job ma dear, am real proud of you. bt nina ombi kama inawezekana kipindi recorded uwe unatuwekea youtube au hapa ili tulio nje ya Tza tuweze kuona pia ni ombi tu. all the best and God bless you.

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: