WATU 18 WALIOCHANGIA MAENDELEO YA MWANAMKE KTK KUFANIKISHA SEMINA DAR, 1 NI MWANAMKE, WENGINE NI WANAUME!!!

Published December 18, 2011 by wanawake1

Shukrani za pekee kwa uongozi wa TCRA kwa kukubali kuwa sehemu ya ukombozi wa mwanamke, kwa kukubali kutudhamini ukumbi wao mzuri na wa thamani kubwa sana, uliyowafanya wawe na furaha muda wote wa mafundisho. kwa kweli kinamama wanawashukuru sana walilia machozi pale tulipowapa ujumbe wa sapoti kubwa kutoka kwenu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA. Pia wanashukuru wafanya kazi mmoja mmoja kwa jinsi walivyoweza kujitoa kwa hali na mali, Mungu arudishe mara dufu pale mlipotoa…walichoahidi ni kufanya yale waliyofundishwa ili wawe chachu ya mabadiliko kwenye jamii, ambapo lengo letu ni kutokomeza UJINGA, UMASKINI, NA MARADHI kwa kasi inayolingana na hali yalisi ya Teknohama……

1. William Laiser – TCRA                             50,000/=

2. Wilfred Maro – TCRA                              50,000/=

3. Fransis Msungu –  TCRA                         50,000/=

4. Alinamuswe Kabungo – TCRA                 100,000/=

5. B.A. Haule – TCRA                                 30,000/=

Pia shukrani za dhati tena ni kwa MABALOZI wa wanawake kutoka UCC ambao wapo jengo la TCRA, kwa kuambua kuwa mstari wa mbele katika kumletea mwanamke maendeleo kwa njia ya kumpatia mafunzo yatakayomsaidia kwenye shughuli zake. Asanteni sana MBARIKIWE SANAAAAAA

6. Frank Tilugulkwa -mwajiriwa UCC                 10,000/=

7. Samueli Masasi – mwajiriwa UCC                 10,OOO/=

8. Emmanuel Natalis-  UCC                              2000/=

9. Alinani William – UCC                                   5000/=

10. Bernard Patrice – UCC                                 25,000/=

11. Moses Kehengu – UCC                              8000/=

shukrani nyingine ni kwa Viongozi wa ngazi y kitaifa, Mh Waziri Benard Membe na J.J. Mnyika, kwa kukubali kuwa Mabalozi wa WANAWAKE nchini kwa kuchangia au kuwezesha Semina kufanyika…..

12Benard K. Membe-  Waziri wa mambo ya Nje- 200,000/=

13. John J. Mnyika- Mbunge-                             100,000/=

Kwa namna ya kipekee WANAWAKE LIVE inampa BIG UP Dk Josephine Slaa kwa kukubali kuwa zaidi ya Balozi wa Wanawake, baada ya kuungana na wanawakelive kwenye mapambano ya kumkomboa mwanamke wa Tanzania bila kujali itikadi, dini, hata kabila, wala hadhi ya mtu… Tumeamua kuwa OMBAOMBA kwa ajili ya WANAWAKE WA TANZANIA…

14. Josephine M. Slaa- Mfanya biashara/ Clinic-  100,000/=

Ella, Maro,Komu, Munishi Kinamama wanawaombea sana popote mlipo, kufurahi kwao ni baraka kwenu, tuendelee kuwa pamoja kwenye mapinduzi haya ya kumkomboa mwanamke kimapinduzi… tumeanza na kumpatia maarifa ya kukabiliana na changamoto za uchumi, changamoto za mikopo, siri ya biashara, namna ya kudhibiti pesa, sheria ya biashara, namna ya kufanya masoko, n.k

15. Ella Ngoti-                                                   50,000/=

 16. A. I. Maro – Mr                                       30,000/=

17. Anthony Komu- Sirito Investiment        100,000/=

18. Deogratias Munishi – Bavicha –               20,000/=

     JUMLA                    1,003,000/=       

Unga mkono mapinduzi ya kumkomboa mwanamke kwa kuchangia kufanikisha SEMINA hizi ili ziweze kuwafikia mama, dada, wifi, semeji, bibi, zetu woooote waliopo vijijini….(Bi Suzi ni mwanamke aliyejitambua na kujiamini, leo hii amefanikiwa sana, anamiliki nyumba tatu na gari hapa mjini, Safari ya mafanikio yake ilianzia kwenye mama ntilie…huyo alievaa blauzi nyeusi na amefunga mkwiju kiunoni, HAPO AKIFUNDISHA NAMNA YA KUJIAMINI NA UNAAMBIWA KUJIAMINI KUNAANZIA JINSI UNAVYOTEMBE, UNAVYOONGEA, ULIVYOVAA n.k) Asante Bi Suzi kwa kukubali kuwa Balozi wa WANAWAKE……

MTAALUM ANAKWAMBIA KUISHI NI KUCHAGUA, KUWA MASKINI AU TAJIRI.. WEWE NDO UTAAMUA!!! KAMA WEWE NI TAJIRI SABABU NI WEWE, NA KAMA WEWE NI MASKINI SABABU NI WEWE…. KAZI KWAKO

UNAAMBIWA ELIMU YA DARASANI BILA KUJALI UMEVUKA VIDATO KIASI GANI, INACHANGIA 1% TU KATIKA MAFANIKIO YA MWANADAMU! 99% NI JUHUDI ZAKO ZA KUTAFUTA TAARIFA NA KUPENDA KUJIFUNZA KAMA UNAVYOPENDA KULA CHAKULA. PENDA SANA KULISHA UBONGO WAKO….(matajiri wengi duniani hawana elimu ya darasani, elimu yao ni ya kujifunza ktk maisha, WanawakeLive Joyce Kiria ndiko anakoelekea, alianza kufanya kazi za nyumbani housegal na sasa ni mtangazaji mkubwa Tanzania anairusha vipindi Afrika Mashariki na Afrika nzima kupitia DSTV) USIBAKI NYUMA…..

WANAWAKE WENGI TUNAPOTEZA MUDA MWIGI KUUGUZA MARADHI YANAYOTOKANA NA MAZINGIRA MACHAFU, HIYO NAYO NI SABABU NYINGINE YA WANAWAKE KUWA MASKINI. NI LAZIMA TUANZE KUJIJENGEA UTARATIBU WA KUSAFISHA MAZINGIRA YETU ILI TUEPUKANE NA MARADHI YASIYO YA LAZIMA….

UNGA MKONO KWA KUCHANGIA TSH 50, AU TSH 100, CHOCHOTE UTAKACHOGUSWA ILI HARAKATI HIZI ZISIRUDI NYUMA – MPESA +255 753 787 126- CRDB 0150258750600

Advertisements

One comment on “WATU 18 WALIOCHANGIA MAENDELEO YA MWANAMKE KTK KUFANIKISHA SEMINA DAR, 1 NI MWANAMKE, WENGINE NI WANAUME!!!

 • ningependa kama ungefanya editing ya rangi, wengine tuna matatizo ya macho, so background ingebaki vilevile ila maandishi yawe na rangi ya kuonekana vyema kama nyeusi kabisa au any which will suit, ni mtazamo tu, thanx

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: