MSAADA TUTANI…….

Published January 6, 2012 by wanawake1

Hello Super Woman Joyce Kiria,

Kwanza Heri ya Mwaka mpya, pia hongera sana kwa harakati zako za dhati katika kumkomboaMwanamke kimaendeleo zaidi.

Kiukweli jitihada zako zinahitaji support ili malengo yafikiwe kwa wanawake wote, na kwa kutambua hilo leo hii

nimesukumwa kukutumia email hii ili at least tuongee na kubadilishana mawazo na wadau wengine na kujua kinachoendelea.

Kuna baadhi ya watu mimi wananishangaza sana tena sana mpaka nashindwa niwaelezee vipi, Kweli kila mtu ana uhuru wake

katika kutumia mitandao the way anavyotaka, ila kweli kabisa  katika zama hizi ambazo wanawake tunahitaji kujikomboa zaidi kimaendeleo

kwa hali zote kabisa,wewe mwanamke unakaa chini na kutumia muda wako mwingi katika mtandao na kuanza kudiscuss maswala ya ndani

kabisa..ninapoongea ya ndani namaanisha ya chumbani,kuna group katika facebook kabisa wamekaa wanadiscuss kabisa uvaaji wa shanga,

Narudia ni uhuru wa mu kufanya wanachokitaka katika mitandao, lakini sidhani kama tunautumia uhuru huu upasavyo, Why tusijiunge na Joyce kiria

katika mapambano ya kumkomboa mwanamke hata kwa mawazo jamani, kuliko hivi kutumia muda mwingi kudiscuss mambo ya chumbani mtandaoni

JE TUTAFIKA KWA MTINDO HUU?

Labda  nimeova react kwa hili, please wadau wa blog hii tuchangie mawazo hii inakuwaje?

Joyce nakuomba jina na email yangu viwe kapuni..

Advertisements

10 comments on “MSAADA TUTANI…….

 • Hauja overeact Joyce…wonders will never end am telling. Kwel hata mimi nashidwa kuelewa kabisa,ndiyo ni uhuru wa mtandao lakin wanawake tunahitiji kujitambua sisi ni kina nani na tunapaswa kufanya nin na kwa wakati gani na sehemu gani. Mimi naamini mwanamke ni jeshi kubwa sana pale anapoamua na kujitambua,hebu tutafute magroup ambayo ni msaada kwetu kimaendeleo,magroup ambayo yatakupa mtazamo mpya kiakili na fikra. Ninachoamini hamna mwanamke asiyejua mapenzi hayo yapo nayataendelea kuwepo,tudiscuss vitu ambavyo ni adimu kuvipata mpaka ushare na wenzio na ujue wanawake wenzio wanawaza nini juu ya kujiendeleza na kujikomboa katika maisha ya kunyanyaswa na mfume dume hasa kielimu,kibiashara,kikazi,kiuongoz nk. Women w need to change coz w cn make it to where w want. Thank u Joyce kuwa mwanamke jasiri na wakuigwa. God bless u

 • Sasa Joyce huyu mdau wako kama anataka mambo wa kuwezesha wanawake kwa nini asianzishe group yake,sisi wanawake tuna matatizo sana na midomo mirefu mmno,

  tena umeover react sana wanawake tumekalia kuezeshwa kila siku hivi hatuwezi kukaa tukatafakari bila kupiga mdomo,haya wewe tangu umeanza kuwaza hayoi umewasaidia wangapi,?na hii domo unalopiga hapa wanawake wakijijini watapataje ujumbe,mi naona nenda katoe magazetini ili kiherehere chako kikuishe,

  hebu tuwe kama wanaume tupunguze midomo jamani,mi huwa naangalia wanawake live lakini sijawahi hata kuona cha maana bora ile segment moja ya mitaani.

  we mdau punguza kiherehere kabla haujapublish kitu fikiria kwanza

 • Kama ushaona wewe wanaongelea upuuzi why don’t u quit? Au ulivisema umechange anything? Kama ulivoisema we have a lot to deal with basi I think u should find somethibng productive to say

 • mi sijakuelewa bado unataka msaada gani hapa maana hayo maendeleo unayotaka wewe wenzako tayari wanayo na waache wafanye wanavyojiskia we kama una shida na maendeleo yatafute kuliko kuleta upuuzi humu

 • Maendeleo ni vyote pamoja na doa au familia kiujumla ndoa isiposimama hamna maendeleo. maendeleo si pesa tu it includes physical. social. psychological enviroment.

 • naimani kubwa huyu aliyeandika ujumbe huu anamatatizo makubwa sana. Watu kukaa na kujadili ni namna gani wafanye ili waboreshe vitanda vyao sio tatizo. Huo ni uhuru wa kila mtu kufanya jambo lolote alitakalo ilimradi asimkwaze mtu mwingine. Nitalaani mijadala hiyo iwapo itakuwa unamzungumzia mtu fulani na kuleta madhara katika jamii. lakini kama mijadala hiyo haimhusu mtu bali ni wazungumzaji wenyewe si kosa.

  Binafsi hata mimi sioni sababu ya wewe kuandika hili na kulileta kwetu.

  Mdau.

 • Mimi naona huyo aliyejishaua kumtumia Joyce Kiria huu ujumbe ana matatizo. Wewe hulazimishwi kusoma wala kuchangia katika group ambalo unaona halina maana. Sasa jamani akina dada, tusiwe kama watoto tusio na mbele wala nyuma. Sasa labda unavyofikiri ukienda kusema kwa Joyce Kiria yeye atafanya nini? au ndo ili mradi unatafuta umaarufu kupitia kwa mtu. Na bora ulivyojificha maana watu wangekutoa kizazi kama unacho!

 • hajui kwa nini ADAMS na HAWA walifukuzwa ktk bustani ya edeni?mapenzi ndo kila kitu na sio wote wanaojua mn kuna kitchen party,unyago,jandoni na siku tunaambiwa mwanamke mwerevu hujenga nyumba yake ila mwanamke mjinga hubomoa nyumba yake mwenyewe utakazana na teknolojia wakati nyumba yako inabomoka afu unaanza kusema kuna mkono wa mtu wakati mchawi ni mwenyewe au umezoea kutembea na wanaume tofauti tofauti mn huoni faida ya mazungumzo yamhusuyo mapenzi mn wameshakutenda wanaume!before hujandika kitu ebu fikiria mara 2 kina impact gani kwa unayemuandikia mama

 • kama kweli unataka kuwaelimisha hao wanawake nenda kwa hilo group na uandike kinachokukereketa maana hata sielewi msaada unaoutaka kwa joyce have confidence bi dada be open ongea ueleweke kama unataka kuungana na joyce find ther way wisely siyo kwa unafiki sawa,,,,,,,,,,,,,,,,,

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: