Wanawake wenzetu wanakufa nje ya shule ya Benjamini Mkapa k,koo Dar

Published January 10, 2012 by wanawake1

Madhara yanaendelea kuwakumba Wanawake na Watoto wenzetu tangu janga la mafuriko litokee jijini Dar,  wamebatizwa jina la wapangaji na serikali ya Tz na hivyo kutupwa kama taka jalalani.  

Hawa wakinamama wana UJAUZITO miezi tisa, wengine nane! hapo walipo hawana vifaa vya kujifungulia wala hawana nguo za kuwasitiri kama vile kanga kwa ajili ya kumpokea mtoto. wewe kama mwanamke unawasaidiaje? hapo walipo ndo wanapolala , mbu ni wao, jua ni lao, mvua yao!!! je, wanawake tunawasaidia vp?? 

Hawa ni wale wahanga wa mafuriko ya Dar, ambapo wao walikuwa ni wapangaji kwenye zile nyumba kabla ya mafuriko. wao wameachwa hawana pa kwenda ila wenye nyumba wamepewa viwanja mabwepande…. wamekata tamaa mnooo

Watoto hawa bado ni wadogo sana ndo kwanza wana wiki kadhaa, hawajui kinachoendelea zaidi ya kulia kwa njaa, sababu mama zao hawana maziwa kwenye nyonyo zao ya kuwanyonyesha hawa watoto wao…. ni huzuni na uchungu kwa mama unapomshuhudia mtoto wako akilia njaa na wewe hujui ufanye nini ktk janga kama hili, ukizingatia SIRIKALI IMEWAMWAGA haiwatambui.. WANAWAKE wenzangu tunawasaidiaje????

Advertisements

3 comments on “Wanawake wenzetu wanakufa nje ya shule ya Benjamini Mkapa k,koo Dar

 • polen kina mama msikate tamaa kabla hujafa hujaumbika yalowakuta hata wengine yanaweza kuwakuta so kwa wale wenye uwezo toen kwan hz pct wanateseka sana dada endelea na harakati zako pa1sana@joy

 • Super woman(joy)kiukweli nimeumia nilipowaona wanawake wenzangu wanavyopata mateso kutokana na athari za mafuriko(nimetokwa na chozi hasa nilipowaona wale wajawazito na watoto wadogo.JOYCE Your real doing something that help the society in a very wide angle.Ila joy tuwambie wanaume si kwamba tumewatenga hata wao wanaweza kutoa michango yao kwa wanawake waliopatwa na mafuriko.Nikipata chochote nitakutafuta ili niwasilishe.kazi njema katika kuwakomboa wanawake na jamii njima kwa ujumla.

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: