WanawakeLive tunampongeza Bi Shamim khalifu kwa kuwastiri Wanawake wenzetu

Published January 11, 2012 by wanawake1

Super Woman Joyce kiria akiwa amembeba mtoto ambaye ana wiki kadhaa wa wale wakinamama waliokumbwa na mafuriko

Kiss ya upendo zaidi kwa mtoto Farida. 

Wanawake Live akiwa na mmama ambaye ndo yule anayetarajia kujifungua wakati wowote,hapa alikuwa akimueleza Joyce kuhusu kusaidiwa vifaa vya kujifungulia.

Wanawake Live imetoa msaada mdogo kwa huyu mama,ila bado msaada zaidi unahitajika, chonde chonde wanawake wenzagu tumsaidieni huyu mama apate kujifungua salama.

Pia Wanawake Live imewasilisha nguo ambazo zimetolewa na bi Shamimu

Joyce Kiria akiwa na wakinamama wakati wa ugawaji nguo.

Zoezi la ugawaji nguo likiendelea.

 

Wakinamama wakichukua nguo zao hapo

“Hapa kila mtu lazima apate nguo hata km ni moja ili mradi wote mgawane”

Si wakinamama tu hata watoto walipata nguo.

Watoto wakiwa wameshikilia nguo zao katika picha ya pamoja na Super Woman Joyce Kiria.

Joyce Kiria akiwa katika tabasamu kwa kuona wtoto wamepata nguo, japo bado bado msaada unahitajika.

Shukurani za dhati jamani zimfikie dada Shamimu mana hata huyu malaika wa Mungu alipata nguo mbili tatu.

Wanawake live inamshukuru sana sana Bi Shamimu Arifu kutoka PROPERT MARKET CONSULT LTD Mikocheni jengo la arcade au heinken karibu na shule ya feza, yeye ndo ametoa nguo zote hizi ambazo zimefikishwa kwawalengwa leo hii. Wewe pia bado hujachelewa bado mahitaji ni makubwa kama unazo nguo za kupunguza kabatini kwako tuwasiliane ili kupata kuwafikia walengwa, hata kama umebanwa na kazi Wanawake Live itazifuata ili kuzipeleka.

Advertisements

2 comments on “WanawakeLive tunampongeza Bi Shamim khalifu kwa kuwastiri Wanawake wenzetu

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: