SERIKALI HII IMELAANIWA, MWANAMKE AZALIA BARABARANI CHINI YA MTI NJE YA SHULE YA MKAPA

Published January 23, 2012 by wanawake1

 

Mama BAHATI ni mmoja kati ya wahanga wa mafuriko  wanaosota nje ya shule ya Mkapa kutokana na SERIKALI kuwanyanyapaa na kuwaita wapangaji ilihali janga wamepata wote. Mama BAHATI alikuwa mjamzito na sasa amejifungua mtoto wa kiume, kwa ushujaa wa mama huyu pamoja na shurba anazozipitia za kulala nje na kuzalia nje bado amempa mtoto wake jina lenye matunaini, BAHATI… Hongera sana mama Bahati , wewe ni shujaa na umedhihirisha kwamba mwanamke ni MAMA anaetakiwa aheshimike bila kujali hali aliyonayo au hadhi aliyonayo..

WanawakeLive tulikuwa tumekamilika, hii ndo team yangu ya kutoa mafunzo mbalimbali yakiwepo ya ujasiriamali na jinsi ya kupata mikopo na kuitumia na kuwaunganisha na mabank, maswala ya sheria, stadi za maisha, kujitambua wewe ni nani na unapaswa ufanye nini kwa wakati gani, namna ya kukabiliana na changamoto bila kujali ni kubwa au ndogo, bila kujali mazingira uliyonayo n.k….

Ringo Mowo akitoa somo kwa waathirika wa mafuriko ambao wanaishi nje, namna wanavyotakiwa kuikabili changamoto waliyonayo na kuanza maisha upya. INAWEZEKANA

Bi Suzy ni mtaalam wa saikolojia, nae akitoa maneno ya kuwatia moyo na jinsi ya kuanza maisha upya 

Simon Rusigwa, nae aliwasisitiza wahanga kwamba MAFANIKIO YA MTU YANALETWA NA MTU MWENYEWE, wanapoendelea kukaa pale nje hawamkomoi yeyote zaidi ya kujikomoa wao wenyewe. ni wakati sasa wakubali kuanza upya, midhali wana afya, hawakufa wala kupata ulemavu basi inawezekana kabisa kuanza upya…..

walitoa baraka zao kwa watoto hawa, waje kuwa mabilionea wa kizazi kijacho

Baada ya kuwafundisha namna ya kuvua SAMAKI walifurahi sana na walibadilika mitazamo yao ya awali ambayo ilikuwa kuendelea kuisubiria serikali, na wakajizatiti wataanza maisha upya wakitumia elimu tuliyowapa. Shukrani kwa Team ya Wanawake live ambao wanajitolea kuleta mapinduzi kwenye Taifa hili….

 


 

 

Advertisements

5 comments on “SERIKALI HII IMELAANIWA, MWANAMKE AZALIA BARABARANI CHINI YA MTI NJE YA SHULE YA MKAPA

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: