MAFUNZO YA WANAWAKELIVE KUWAUNGANISHA WAJASIRIAMALI NA MABANK ILI KUPATA MIKOPO

Published January 27, 2012 by wanawake1

Mafuzo ya Wanawakelive tumeyaboresha kwa kuwaunganisha wajasiriamali na BANK mbali mbali ili waweze kupata mikopo ya kuendesha ama kuanzisha biashara ili kujiletea maendeleo zaidi….

Strong Woman Joyce Kiria akifungua semina

Ringo Mowo mwalimu na muwezeshaji kwenye semina

Dk Josephene Slaa balozi wa WanawakeLive….

Hiyo ndo timu ya kujitolea ya Wanawakelive  inayofanya semina za kuwaendeleza wanawake, Joyce Kiria, Ringo Mowo, Josephene Slaa na Bi Suzy…

Anafanya biashara mbalimbali kama kuuza mboga mboga, maandazi, chapati, viatu, vitenge n.k   kupitia semina ameshasajili kampuni ya ukandarasi na anatarajia kupata mkopo ili afanikishe ndoto yake ya kuwa Bilionea… INAWEZEKANA

Amesomesha watoto kwa biashara ya chapati hadi kufika chuo kikuu, kupitia semina amejua ni jinsi gani ya kujiendeleza zaidi 

Alikuwa anauza vitu kwa kuzunguka ”mmachinga” Baada ya kufanya nae kipindi cha Wanawakelive na kubadilishana uzoefu na wanawake waliofanikiwa ,leo amefikia hatua ya kukodi fremu na biashara yake inazidi kukua, na sasa semina zinaendelea kumpa mbinu zaidi za kupiga hatua mbele….

Wanawake wakishuhudia namna mafunzo haya yalivyokuwa chachu ya mafanikio na tayari wameshaona mabadiliko..

Tukifuatilia mafunzo yatakayobadilisha kabisa maisha yetu….

Bi Suzy ni  Mshauri yupo katika timu ya ukombozi wa mwanamke kwenye Wanawakelive, amebobea zaidi kwenye saikolojia, ni mwanamke anafundisha masomo ya kujiamini na kujitambua kuthubutu n.k….

Dk Josephine Slaa katikati ya Waathirika wa mafuriko ”wapangaji” wanaoishi nje ya shule ya B. Mkapa nao walipata fursa ya kujifunza zaidi jinsi ya kuanza maisha na kufanikiwa ,  majaribu yanakuja kutokana na sababu , yawezekana bila mafuriko wasingepata elimu wanayoipata ambayo itaenda kuwabadilisha kabisha na kuwa mabilionea wa siku zijazo….

 

28 jan 2012 tutaendesha semina nyingne kwenye jengo la TCRA , pamoja ba semina tumewaalika Bank ya Wanawake TWB na Stanbic Bank ili watoe mikopo kwa wahitimu wetu ambao wataonekana wameelewa na wataweza kufanya biashara na kurudisha mikopo…

Tumeshaongea nao na kwa upande wa bank ya Wanawake atakuja mkurugenzi Mama Magreth Chacha, na upande wa Stanbic atakuja Johari Kelvin ambapo yeye ni Business Banker..

Ni wakati wako wa kujiletea maendeleo kamwe usikubali kubaki nyuma..

WANAWAKELIVE NI MAPINDUZI YA MWANAMKE/ MAENDELEO YA MWANAMKE/ KWA KILA MWANAMKE…

TUNAWASHUKURU SANA TCRA KWA KUSAPOTI MABADILIKO HAYA KWA KUTOA UKUMBI WAO BURE KABISA

 

 

Advertisements

4 comments on “MAFUNZO YA WANAWAKELIVE KUWAUNGANISHA WAJASIRIAMALI NA MABANK ILI KUPATA MIKOPO

 • hi Joyce

  Hongera saana kwa kutufungua macho na masikio mienilitaa kufaaa utaatibu wa kuja kwenye mkutano huu unakuwaje,coz sijawahi kushiriri nilitaka kujua na kupata darasa.

  Uendelee na moyo huo huo wa kutukomboa waawake

 • Umenipa faraja kweli Sister Joyce coz nilikuwa nahitaji sana kitu ambocho nakiwaza siku zote kwenye akili yangu kiweze kutamkwa live kwenye kinywa cha mtu mwingine na hasa kama wewe. Kitu kilichonitia moyo ni hapo uliposema kwamba mnasaidia watu kupata mikopo inamaana mnamuwezesha mtu nilichokuwa naomba ni kwamba niwe na uwezo kwanza wa kuhudhuria seminar zenu huku nikiendelea kutafuta mtaji maana ndio niko kwenye harakati za kuutafuta. Naomba tutaharifiane ni lini tunakutana tena kwenye hiyo seminar hili nijiunge rasmi kwenye crew yako.

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: