MKURUGENZI WA BANK YA WANAWAKE TZ ATEMBELEA MAFUNZO YA WLIVE

Published January 31, 2012 by wanawake1

Haya mafunzo yamefanyika jmosi 28jan2012 kwenye ukumbi wa TCRA, ni mafunzo ya kumwendeleza mwanamke bila kujali itikadi wala kabila, hadhi, na kila aina ya tabaka….

Strong Woman Joyce Kiria akifungua mafunzo ya kumkomboa mwanamke kimapinduzi ktk ukumbi wa TCRA barabara ya Sam Nujoma …

Super Woman na Mkurugenzi wa Bank ya Wanawake Tz Mama Magreth Chacha akizungumza na wajasiriamali na kuwafundisha mbinu za kupata mikopo huku akiwaahidi kuwapa mikopo endapo watazingatia mafunzo wanayopata, pia alisisitiza kwamba UMASKINI wa mtu huletwa na mtu mwenyewe na kuwahimiza wjizatiti kuondoka kwenye umaskini kwa kuwa INAWEZEKANA..

kwa maneno mengine ni kwamba kama mtu hajakuwa tayari kuuaga umaskini basi hata umfundishaje hatang’oka ng’o.. hata um’bebe na winchi hatabebeka, kwa hiyo kabla hujaja kupata mafunzo kwanza jiulize umejiandaa kuachana na umaskini?? umaskini ni ugonjwa unaotibika lakini tiba ya kwanza inatoka kwako.

Mwalimu wa semina zetu Ringo Mowo akiendelea na ratiba ya kutoa mafunzo katika mkutano wa jmosi iliyopita. semina ilianza kwa kupata shuhuda kwa baadhi ya watu ambao tayari wameshachukua hatua za kuuacha umaskini

Safari hii watu walifurika sana, ukumbi haukutosha, tupo kwenye changamoto ya kupata eneo kubwa zaidi …

Arafa Arobaini ni mjasiriamali aliepiga hatua baada ya kufatilia kipindi cha Wanawakelive msimu wa kwanza, kwa sasa anazidi kuendelea mbele na hapo alimkabidhi Super Woman zawadi za nguo alizotengeneza mwenyewe, kofia , sketi, nguo za mtoto wa Joyce Kiria…

jmosi ya 04/02/2012 semina itafanyika Ustawi wa Jamii barabara ya sinza (BAMAGA) na jmosi ya 11/02/2012 kutakuwa na semina ya watu wote.. endelea kututembelea ili ujue itafanyika wapi….

SHUKRANI KWA TIMU YA MABADILIKO HAYA , RINGO MOWO, JOSEPHINE SLAA, SUZAN MREMA, MWANASHERIA WETU DADA GRECY….

Advertisements

4 comments on “MKURUGENZI WA BANK YA WANAWAKE TZ ATEMBELEA MAFUNZO YA WLIVE

 • Nakupenda joyce kria jamani mbona umetutupa wachaga wenzako napenda kuwa mjasiria mali kuuza vyombo vya mtumba niuinganishe wangu karibuni moshi kanyi

 • Leave a Reply

  Fill in your details below or click an icon to log in:

  WordPress.com Logo

  You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

  Google+ photo

  You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

  Twitter picture

  You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

  Facebook photo

  You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

  w

  Connecting to %s

  %d bloggers like this: